Maria Zakharova ameashiria madai ya nchi za Magharibi kwamba zinafanya juhudi kurejesha amani huko Ukraine na kusisitiza kuwa: "Hatua hii ya Magharibi inakinzana na matamshi ya nchi hizo."
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kuwa, nchi za Magharibi zinafanya kila kinachowezekana ili kuchelewesha oparesheni amilifu ya jeshi la Russia nchini Ukraine.
Christine Lambrecht Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani jana Jumanne alisema kuwa, Berlin itatoa kibali cha kuikabidhi Ukraine vifaru; hatua inayodhihirisha kubadilika wazi sera za tahadhari za Berlin katika suala la kuiunga mkono kijeshi serikali ya Kiev.
Wakati huo huo Ufaransa pia inatazamia kuipatia Ukraine makombora ya Caesar yenye uwezo wa kupiga umbali wa kilomita 40 huku Uingereza nayo ikiwa tayari imeipatia Kiev makombora ya Starstreak.
342/